KUHUSU SISI
Home About Us

HISTORIA FUPI YA CHUO

Chuo cha Ufundi Ifunda Mission kilianzishwa mwaka 1995 chini ya Muasisi wake Hayati Fr. Alfons Mhamilawa (Mwenyezi Mungu ailaze roho yake mahali pema peponi, Amina).
Fr. Alfons alipata wazo la kuanzisha chuo cha ufundi baada ya kuona wasichana wengi wanakosa fursa ya kusoma au kutopata nafasi za kuendelea na masomo zaidi. Hivyo wengi wao kubaki nyumbani na kushawishika kuingia kwenye ndoa change na wengine kujiingiza kwenye tabia zisizo njema. Hivyo alitamani kuona wasichana hao wakipata ujuzi kupitia chuo chake.
Kozi ya kwanza kuanzishwa ilikuwa ushonaji. Mpaka sasa chuo kina kozi takribani sita na wanafunzi wasiopungua themanini. Hakika maono yake yamekuwa mema sana.

KUHUSU CHUO

Ifunda Mission Vocational Training Center ni chuo kilichosajiliwa na Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi (NACTE) - Tanzania; Kikiwa na namba za usajili VET/IRA/PR/2018/C/101 ili kutoa mafunzo ya ufundi stadi kwa ngazi ya cheti. Tangu kuanzishwa kwake, chuo kimekuwa kikitoa mafunzo stahiki katika kozi zake na kimeendelea kukua zaidi kadri muda unavyozidi kusogea. Baadhi ya mafanikio yanayojiviniwa na chuo ni kupanua wigo wa mafunzo kutoka kilipoanzishwa kikiwa na kozi moja hadi saa ambapo kinatoa kozi sita pamoja na kozi ya ziada ya Computer Application.
Chuo kipo umbali wa mita 500 kutoka barabara kuu ya kutoka Dar – Mbeya. Barabara zake zinapitika misimu yote kiangazi na Masika.

Core Values

 • Creativity
 • Hardworking
 • Team work
 • Transparency
 • Integrity
 • Honesty


Our Mission

 • Being a committed and hardworking team of people that work together to build our school.
 • Introducing quality business that assist in making a profit for the school in order...
 • Working and sharing with relevant and similar partners in order to ensure that we benefit together.
 • Ensuring that we make use of any waste product from our business and school so that we respect our environment with no risk to our own people.
 • Reducing the amount of school fees in order to help impoverished youth to join the school

Our Vision

  Providing quality education and training so that all its student are either employed in decent jobs or are competent enough to open their own successful business. While ensuring the above, the school, with its own business, well work toward becoming self - sufficient to cover its operating cost.

MIRADI YA CHUO

DUKA
UFUGAJI NGURUWE
NYUKI
KUKU WA KIENYEJI
MGAHAWA

MAFANIKIO YA CHUO

>> Tumefanikiwa kukuza mradi wa ufugaji wa nguruwe kutoka nguruwe wanne (4) tulioanza nao mpaka kufikisha nguruwe thelathini (30)
>> Katika taaluma wanuchuo wetu wamekuwa wakifanya vizuri mitihani ya taifa na baadhi yao kuajiriwa katika mashirika makubwa kama Tanesco nk.